MJADALA: WANYAMA WA NDANI (PETS)

Wadau wangu narudisha tena hili shindano kwa hisani kubwa ya mdau mkuu wa blog hii JJJJJJJJJJJJJJJJJB, nimeona niweke picha ya paka kwani, wengi wetu hapa Tanzania tunatufuga paka, jamani apatikane mshindi kuchukua kitita hicho...

Mashughuli blogspot ikishirikiana na JB, mdau mkubwa wa blog hii inapenda kukaribisha mazungumzo wa wazi kuhusu wanyama wa ndani (PETS), kwa kila mmoja atakae taka kuchangia kuhusu swala hili na jinsi gani watanzania wanavyo liangalia kwa ujumla. Masharti ni kama ifuatavyo:-

- Jinsi gani walivyo kua na faida kwetu na familia zetu kwa
  ujumla.

- Tufanyaje ili tuweze kufaidika kwa kuwanao bila
  kuwatumia kama walinzi au njia ya kulinda panya katika
  nyumba zetu.

- Je tunaweza kubadilisha uhisiano wetu kati ya wanyama
  tunaoishi nao kutoka katika ulinzi kuwa marafiki zetu au
  hata member wa familia zetu.

- Wanyama tutakao anzia kuangalia ni Mbwa, Paka na
  ndege.

Unachotakiwa kufanya ni kuandika at least 2 page maneno yaziyozidi 200 kuelezea jinsi gani uko karibu na mnyama ambaye unaishi naye ndani ya nyumba, pia ambatanisha picha tofauti ukiwa pamoja na huyo mnyama.

Baada ya washindi 3 kupatikana tutawafuatilia kwa karibu kwa kipindi kifupi ili kupata mshindi wa 1,2 & 3

Mshindi atajipatia fedha taslim 100,000/= toka kwa mdau wa blog hii JB

Tunacho jaribu hapa ni kuanzisha muamko kwa Watanzania jinsi gani tunavyotakiwa kuwalea na kuwajali viumbe ambavyo tumevinyaganya uhuru wao na kuwaweka katika majumba yetu kwa faida yetu hivyo wanahitaji mapenzi, malezi na kutambua umuhimu wao duniani na jinsi gani wanaweza kutuletea furaha, faraja hata kutulinda au kutushtua katika ajali ambayo hatuioni au hatujui kama iko karibu yetu au hata kutuokoa katika hatari

Nina hakika inaweza kuchangamsha mazungumzo na uelevu kwa watu na kuweza kuheshimu na kumuona Mungu kwa karibu zaidi na kusifu uhodari wake kwa kila kiumbe chake.

KUMBUKA KILA KIUMBE KINA HAKI YA KUISHI, KUHESHIMIWA NA KUDHAMINIWA.

Post a Comment

0 Comments