MASHUGHULI BLOG INATOA POLE KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR
Mashughuli Blog inatoa pole kwa familia za watanzania 13 waliopeteza maisha yao katika mafuriko makubwa yaliotokana na mvua ambazo zimekuwa zikinyesha tokea juzi Jumanne Desemba 20, 2011, Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amina. Pia Mashughuli Blog inatoa pole kwa walioumia na kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Pia tunalipongeza Jeshi la Ulinzi kwa kusaidia uokoaji na kulinda mali za wananchi na kuwapa wananchi muongozo. 
Watanzania, waathirika wa mafuriko wanahitaji michango yetu kwa hali na mali kwa chochote kile ulichojaaliwa, magodoro, maji safi, chakula, nguo za watoto na watu wazima nk, kwa sasa waathirika hao wamejikusanyika shule mbalimbali za msingi na sekondari, vituo vya kupeleka misaada hiyo kwa sasa ambavyo vinajulika ni :-
- Azania Sekondari
- Magomeni
- Msimbazi
- Mchikichini
- Kibasila
- Magomeni
- Uhuru mchanganyiko
- Hananasifu

kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments