SALAAM ZA MWAKA 2012 - MASHUGHULI BLOG

Mashughuli Blog inapenda kuwatakia kheri ya mwaka mpya 2012  wenye mafanikio wadau wote wa mashughuli blog, pia kutoa shukrani kwa watu wote ambao wananisupport kwa njia moja au nyingine, ni wengi sana ambao ninawafahamu na nisiowafahamu nawashukuru sana. Ningependa kawapa shukrani za pekee hawa wafuatao kwa kuwa karibu na mimi haijalishi wako wapi katika hii dunia bali wako nami kwa kila jambo hata pale ninaposhindwa huniinua kwa mikono miwili, naamini kuna mazuri na mabaya kwa mwaka 2011, Basi iwapo nilikuudhi au kukukera kwa kusudia au pasipo kusudia naomba tusameheane pia ninaamini tunajifunza kutokana na makosa, kwa jambo lolote ambalo umependa, hujapenda, hujaridhika nalo, una dukuduku au ushauri wowote wa kurekebishana usisiste kuwasilinana nami kwa email kupitia MASHUGHUILI 
Shukrani

Kwanza tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa uongozi mzima wa Manzelline Quality Centre Mall &  Shoppers Plaza kwa kudhamini Mashughuli blog.

Pia naishukuru TMH chini ya uongozi wake Khadija Mwanamboka, kwa kuitambua Mashughuli blog na kazi zake kwa jamiii, Nimemjua Khadija tangu nilipoanzisha blog hii  ingawa  nilikuwa namfahamu zamani kama Designer maarufu lakini yeye hakuwa ananijua mimi.  Tumefanya naye kazi kwa muda mfupi, lakini ameona mchango wetu na ndio maana TMH wakatuzawadia hii "Certificate of Appreciation."  
Joha Simba Abdallah - Yeye ni Mbunifu mkongwe, Mkuregenzi wa JOHAB Tailoring Mart iliyopo Upanga Dsm, jamani sijui nianzie wapi  kuhusu huyu dada. Inatokea kuna watu unawajua halafu unamshukuru Mungu kwa kukutanisha nao. Kwa watu kama hao, basi kwangu mimi huyu ni mmoja wao kwa upendo, ukarimu aliokuwa nao yeye na mume wake Bwana Abdallah. Dada Joha hapendi kuniona nimenuna kabisa atafanya juu chini nicheke! Asante dada Mwenyezi Mungu akujaalie miaka mingi na afya tele!!
 
Said & Batul (Mr & Mrs), Ni kaka na supporter kuanzia siku ya kwanza. aliona picha ninazorusha mara ya kwanza sio nzuri basi Batul & Said walitenga kiasi cha fedha kuninunulia Camera ili niweze kupiga picha nzuri, Camera hii ninayofanya nayo kazi imetoka kwao na wananisaidia kila siku ingawa wako mbali. Tahiya Dawood, mjasiramali - supporter wangu na rafiki yangu huwa 
namuita mdau namba moja wa Mashughuli Blog.
 Nuru Mwene - Sister & Supporter, she is a loving mama jamani, i am so glad to know her!!
 Farida Simba Mtengeti - Development Consultant - Sister & mshauri wa blog, yeye ndio wa kwanza kunishauri nifungue blog itakayohusiana na shughuli zetu za kiswahili ambazo mara nyingi mimi huwa mmoja wa wahudhuriaji, na ni mshahuri mkuu wa Mashughuli Blog,

 MC Jamila Kitimtim - friend & supporter, huyu ni mc lakini katika kila shughuli huchukua japo dk 3 kuielezea Mashughuli Blog ni nini. kwa wale ambao hawanijui wanapata muda wa kunijua na huwa tayari kwa camera kwa ajili ya picha na pozi!

 Salma Mntambo, Injini ya jiji - si unajua ukisema mama basi huyu ndiye mama anayeheshimu kazi ninayofanya na kunisupport yeye na familia yake. Sijui nianze wapi  kumuelezea huyu mama mwenye upendo kwangu binafsi na Mashughuli Blog na hata katika mbali na blog.
 Dada Fatmah Simba , yeye ni mama wa fedha, anakikisha kuwa Mashughuli Blog inaingiza pesa. Ukiona tangazo humu ndani basi ni yeye kachangia kuhamasisha wadhamini kutangaza kwa Mashughuli Blog. Thanks my dada may God bless you and your family.
 Tanti Boy somo wa ukwe'ee - jamani si mnakumbuka mambo yake akiwa na mwali mambo makubwa, sasa yeye akiwa na shughuli yake lazima Mashughuli Blog tukachukue matukio, thanks my dada..!!!
Mariam & Tindwa,- kama mnavyowaona hawa ni Mntambo Family ni supporter wangu kweli kweli, like mama yao Salma Mntambo.
Alliyah! - Supporter 
My college mate Nuru Milly Mkeremi - Supporter & rafiki mpenzi. 

Hellen - Mashughuli Blog
Post a Comment

2 Comments

  1. Jamani Miriam Aziz Hayupo hapa?!mmmmh haya wacha nipite.

    ReplyDelete
  2. hongera sana wajina wangu..kazi nzuri na nakutakia 2012 wenye baraka na mafanikio zaidi na zaidi..

    ReplyDelete