KADI YA MUALIKO (Invitation Card) UMUHIMU WAKE KATIKA SHUGHULIUmuhimu wa kadi za mwaliko katika shughuli zetu za kila siku, je ni yapi ya kuzingatia katika kutayarisha kadi ya mwaliko? au unatengeneza kadi kwa sababu fulani kwenye harusi yake alitengeneza kadi ukaipenda?, mimi naamini kila mtu ana hisia tofauti za furaha ua huzuni, umuhimu wa kwanza ya kadi ya mualiko ni kuwapa waalikwa ili waweze kuhudhuria sherehe iliyokusudiwa na pia wapate ufahamu wa dress code, muda wa shughuli inaanza saa ngapi? na infomations mbalimbali, ni heshima kumpa mualikwa kadi, kwani inawezekana kabisa ukamwambia kwa mdomo na akaitikia wito wako, pia ni kielelezo muhimu cha kuelezea hisia zenu au zako za furaha katika sherehe yako hapa ninamanisha picha na marembo ya kwenye kadi, mfano wa kadi hapo juu kuna picha ya ndege tausi, wengi twamjua na kumpenda ndege huyu, kwa mlengwa wa sherehe anatoa hisia zake kupitia ndege huyu wa tausi, kadi ya mwaliko husaidia sana kuweza kucontrol idadi ya wageni katika sherehe ili uweze kumanage vinywaji na chakula vilivyotayarishwa, mimi mara nyingi uwa nasema hakuna sherehe ndogo kadi ni muhimu sana katika kajishughuli unachokiandaa.

TABLE NUMBERS & MENUS
Je na hizi nazo zina faida gani?? maana usifanye kitu bila kujua umhimu wake mimi sipendi gezageza kwa sababu fulani kafanya kwenye shughuli yake basi na wewe unafanya. 

TABLE NUMBERS
Hizi zinasaidia kuwapanga wageni katika makundi wanayofahamiana ili waweze kusherekea kwa ukaribu zaidi, siku hizi tunaona watu wengi wakienda shughulini anaanza kumtafuta shosti kakaa meza gani ila wawe pamoja au unakaa meza na watu hamuongei mpaka mwisho kwa sababu ya kutofahamiana, hata katika ule mpango wa kupiga picha basi mtapiga picha mashostito pamoja na walengwa pamoja.

MENU
Menus katika shughuli inasaidia waalikwa kujua ni vinywaji au chakula gani vinapatikana katika hiyo sherehe wakati mwingine unakutana ma muhudumu hajui majina ya vinywaji fulani kwa hiyo anashindwa kukuambia, pale muhudumu anapofika tu unakuwa tayari unajua unywe nini, pia wakati wa buffer unakuwa tayari umeshaliandaa tumbo kupokea msosi gani, jamani sio lazima ukienda kwenye buffer uweke chakula chote lakini ukifika mezani unakula vyakula viwili tu, kwanza ni dhambi kutupa chakula so chukua vile unavyoweza kumaliza.

CEREMONY PROGRAMS
Program za sherehi ni nzuri katika shughuli zetu ili kuwapa waalikwa kufahamu kinachoendelea katika sherehe na hata mualikwa akichelewa anajua tukio lilopita na linalikuja ni lipi.

LIST OF VENDORS.
Hawa ni wale wtu waliotoa huduma katika sherehe nzima, wapambaji, MC & mziki, mpishi etc., ni vinzuri ukatafuta kijisehemu hata nyuma ya ceremony program ukawaandika wote kama mpambaji kafanya kazi yake nzuri basi itamsaidia kupata kazi nyingi zaidi na pia itasaidia vendor kuwa makini na kazi zao ili kujiongezea kazi zaidi hii ni ngumu kidogo kwa sababu moja kwa moja itakucost wewe na vendor ni tofauti ni vinzuri tukawatumia wedding planner kwani ni rahisi ya yeye kujitangaza, na hawa vendor watapatikana kupitia yeye.


Wadau changieni mawazo yenu katika hili ili tuelimishane.


Imetayarishwa na Mashughuli Blog


Post a Comment

1 Comments

  1. Sasa mashughuli unaongea point yaani mimi nakushauri uwe wedding planner it seems unaelewa mengi sana

    ReplyDelete