Kulikoni? - Zawadi Fake


Haya wadau wangu hii ni kona mpya ya Kulikoni, wewe kama mdau wa Mashughuli Blog, ningependa utoe  dukuduku lako linalokukera pale unapokwenda shughulini (Send Off, Singo, Kibao Kata, Kitchen Party, bag Party, nk) wadau wengine nao watapata nafasi ya kuchangia kwa kutuma maoni yao na sisi sote tutajifunza kwa njia moja au nyingine!

Zawadi Fake: Najua wengi wao mtajiuliza zawadi fake ni kitu gani? Mimi nimekaa na kufikiria sana ndio maana nikaiita zawadi fake, haswa haswa kwenye kitchen Party au shughuli zetu za kina mama, unakuta mtu anasimama tena ni mwanafamilia na kuchukua microphone na kusema “sisi kama shangazi zake bi harusi tumemzawadia sofas, kwa sababu zisizoweza kuzuilika tumeshindwa kuleta hapa ukumbini basi tunamkabidhi risiti yake” jamani kumbe hakuna zawadi wala chochote ni kujitoa kimasomaso mimi nasema hivi kama huna si basi, mpe bi harusi mkono wa hongera muombe dua njema vinatosha sio mpaka mtu mnzima na akili zako kusema uongo tena mbele ya hadhara, kuna bi harusi niliwahi kumtembelea nyumbani kwake nakumbuka kwenye kitchen party yake, dada zake sio wa tumbo moja walisimama na kusema tumempa zawadi ya sofa ambazo ziko dukani risiti hii hapa atakwenda kuchukua, sasa nilipofika kwake nilikuta sofa za ukwee, na mimi nikamsifia makochi yako manzuri kwa kweli wale dada zako walikupa zawadi nzuri sana!, wacha bi harusi achambe wapi ndugu sikupata sofa wa stuli, hizi ni za kwetu tumenunua mimi naume wangu, nilishngaa sana!!! Wako wazazi wengine wanadiriki kwenda kwenye maduka makubwa wanayouza fanicha na kukodisha ili mradi tu walete ukumbini, ilikuwaonyesha watu eti umefanya shughuli. Kuna kitchen party ilifanyika hapa mjini kama miaka 3 iliyopita ilikuwa pambe ile mbaya hapa mjini kwa sababu mama mzazi anajulikana hapa mjini, baada ya harusi kuisha ikatokea siku marafiki wa bi harusi kwenda kumtembelea mwenzao walishangaa zile fanicha za bei ya gharama zilizokuwa zikionekana pale ukumbini hakuna hata moja????? Inahusu! Kwa nini hatujikuni pale mkono unapofika? Jamani vidole havilingani bado hatuelewi??? Ndio maana uwa nawashangaa sana ukitoa harusi za uswazi watu wanakandia kumbuka kama wewe ni wa hali ya juu, yuko pia mwenye ile harusi naye eye anataka itoke kwenye blog kama yako na kwa uwezo wake, na hayo ndio maajaliwa yake Mwenyezi Mungu kwake!!! Tuwe wastaarabu huna haja ya kujikwanza kwa kusema uongo!!!Post a Comment

1 Comments