NINA UZOEFU NA FANI HII YA MITINDO KWA MIAKA 17, SUPER MODEL MTANZANIA TAUSI LIKOKOLA, MASHUGHULI BLOG YAFANYA NAYE MAHOJIANO, soma upate kumfahamu zaidi

Tausi, Karibu sana ndani ya Mashughuli Blog, Mambo vipi:, tunaomba utupe historia kidogo ya maisha yako:

Tausi: Nilizaliwa Tanzania na kusoma mpaka high school halafu nilienda kwa masomo nje ya nchi....na kuombwa kuingia kwenye fani ya mitindo. Nimekuwa kwenye mitindo zaidi ya miaka kumi na saba.....nilianzia Ujerumani. Kwa hivi sasa ni mama wa nyumbani na ninalea watoto wangu

1. Unakumbuka nini zaidi kuhusu maisha yako ya utotoni? ulitaka kuwa nani? ulipenda michezo gani na tukio gani la utotoni ambalo hutokaa ulisahau?

Tausi: Jamani nililelewa vizuri na bibi, wajomba, baba na ndugu kama hilivyo nyumbani…nilikuwa na utoto wa furaha. Nilifikiri nitakuwa daktari na nilisoma PCB Jangwani niende Muhimbili…lakini nilipata nafasi kuenda nje ya nchi ingawa nilipata points nzuri shuleni nilichagua kuondoka na kujaribu maisha nje ya nchi. Nilikuwa nyumbani wakati Nelson Mandela alipofunguliwa, tulicheza ngoma! 
2. Nikikupa nafasi ya kuwapa ushauri wasichana wadogo(teen girls),ambao wana mawazo ya kuwa model kama wewe, ungependa kuwapa ushauri gani?

Tausi: Sasa hivi sisafiri sana na sichukui kazi nyingi za mitindo bali nachagua chache…na ninawasaidia washichana wadogo wafanikio kwenye mitindo na sehemu nyingine. Kwa kweli wanaotaka mitindo, ili kufanikiwa international inabidi uwe mrefu, umbo dogo na ngozi nzuri…ingawa sehemu nyingine tofauti wanaangalia vitu tofauti. Hivo inabidi wajitunze na kujaribu kuongea na watu hapo nyumbani wanofanya kazi za mitindo ili wapate experience na connections…inabidi kuwa mwangalifu na kufuatilia na familia yako au mentor. Halafu uendelee kwenda shuleni. Kama wanaweza kupata news waende na 'like' facebook fan page yanguhttps://www.facebook.com/pages/Tausi-Likokola-Fans/208895639171155


3.Wewe ni mama, na model je unawezaje kuoanisha au ku-balance mambo yote haya kwa mpigo?Tausi: Kwa kweli unaweza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja…ila watoto wangu wanakuja kwanza halafu napanga kipi naweza kufanya ambacho kitasaidia familia nzima na jamii vilevile.


5. Je na watoto wako pia ni model?

Tausi: Hapana.... watoto wangu ni wadogo . Imani ana miaka mitano na Neema mitatu...... wanapenda kupiga picha nami lakini sijafikiria kujiunga na fani.


Mashughuli Blog -Asante sana Tausi kwa muda wako, kila la kheri katika kazi zako!


Tausi: Ahsanteni na muendelee na kazi nzuri ya kuelimisha jamiiPost a Comment

3 Comments

  1. Aunty mashuguli unatisha duhh hata sijui nisemeje maana ulijipanga na kuuliza maswali mazuri naye amejieleza vizuri. Well done

    Mama Dja

    ReplyDelete
  2. safi sana dada lakini unapo andika naomba usome vizuri uwandikanyo hayo matamshi maana kunakupitiliza dada pole

    ReplyDelete