DIAMONDS ARE FOREVER LIVE CONCERT MILMANI CITY

Kwa ufupi live concert ya Diamond ilikuwa nzuri haijawahi tokea, watu walipendeza kwa kwenda mbele, nenda picha uone jinsi watu walivyolipuka na kupagawa na Diamond, si unajua almasi inatia wazimu pata picha

 Almasi ambayo haichuji thamani yake akiingia na mama yake mzazi


Wema akiingia...!!!


Diamond akiwahi kukiri kwenye Radio 88.4 kipindi cha Diva Loveness kwamba Royal Modal wake ni Q-Cheif hata kabla ya kuanza kuimba na namkubali sana...!!!Steve Nyerere akimtunza Q-Chief

mwaga dollar $$$$$
Zeze ulinoaje sijakupata kwenye RED Carpet
Hapa ndio Wema katolewa nje......!!!
Jamani bado hujamuona Wema???
Haiwezekani
pole bidada...!!!, nasikia chozi lilimtoka Wema

akicheza na JLO & Jokate


Diamond akibembelezwa na Taji Liundi

Vijana wa THT wakamchukua Wema kumpooza......!!!
Twende ukampuzike mami...!!!


watu walifurahi sana.....!!!

Diamond akimuimbia Aunty Ezekiel
Mama akimtunza mwana..!!!Ommy Dimpz nae hakukosa...!!!

Kim KBarnaba nae alimpa support dogo..!!


Diamond Amin & Barnabas
Wema akimtunza Barnaba


Waswahili wanasema wagombanao ndio wapatanao maana visa vyao bwana! hapa Diamond kapanda juu ya meza aliyokaa Wema


Wema na kama hamuoni vile...!!

Nyuso

Mange & Wema pendeza eeh!!!
Diamond akiimba kwa madaha mbele ya Wema

Mange & Kisa
Kim K, Halua & Ommy Dimpoz

Red Carpet
Kim K

Kim & Halua
Janeth Sosthenes 


Sauda Mwilima wa STAR TV
Shaa kati na marafiki


RIO
Queen Dalila & Friend
Janeth akiendelea kuwahoji watu ndani ya RED CARPET mavazi yao!!Mange & Remtula
AuntyMartin Kadinda Single Button Blazzer zatawala kwenye concert 
Amin pozi nyingi...!!!Colour blocking 
SWAGA
Post a Comment

17 Comments

 1. uwiiiiiiiii jamani watu wamependezaaa sana kwa kweli mliienjoy,..pole dada wema kwa aibu hiyo lakini usijali huyo diamond atapata vikaragosi tu hata pata mwanamke mrembo kama wewe na pia elewa hizo ni fitina tuu za watu wanamfanya awe hivyoo ,amini usiamini huyo ni wako wa milele nakushauri wewe tulia tuu.

  ReplyDelete
 2. Weanonymous hapojuu, mwanamke sio urembo peke yake, hata tabia pia yatakiwa. Wema alimtukana sana diamond eti ni nuksi, mlitaka kijana wa watu afanyeje< apokee hela ajidharirishe.

  ReplyDelete
  Replies
  1. HATA KAMA KAKATAA KUPOKEA JE WEMA SI AMETOA HELA YA KIINGILIO NA HIYO PIA SI AMEPOKEA YEYE KAMA KWELI HAMTAKI ANGESEMA HATAKI KUMUONA KWENYE SHOW YAKE KABISA, UPUUZI MTUPU,WEMA FAN

   Delete
 3. Asante..... Endelea kufanya kazi nzuri Mashughuli!!

  ReplyDelete
 4. ht km walikuwa wanabif zao haikutakiwa kuonyeshana kazini, diamond alikuwa kazini hakutakiwa kuweka mapenzi Wema alikwenda pale kama fan wa diamond alitakiwa apokee si kuendeleza libeneke la bif lao, hii inaonyesha kwamba hana heshima kwa mwanamke km kweli anamweshimu mama yake why ashindwe kumweshimu wema anataka kuniambia Wema ni kwamba hajawahi kumfanyia mazuri yeyote hd amwanike kiasi hiki, mi navyoona bado anafeel sema tu anafanya mgumu ili amplease Jokate ila ht huyo Jokate asidhani kwamba kwa mwenzie kufanyiwa hivyo yeye itashindikana kufanyiwa hivyo haina haja ya kuachana na kufanyiana action za ajabu kiasi hicho mi nilikuwepo ule mi naona ni uswahili uliopitilia, the show was good ila amejiharibia mwenyewe baada ya kushiba sifa mwisho wake akaharibu, me am on Wema's side sijaona kosa lake kwa usiku ule aliguswa kwa wimbo km alivyoguswa fans wengine akaamua kutunza whether walikuwa na ugomvi au laa haikuwa party of the show...

  ReplyDelete
  Replies
  1. Whoever you are, you are very right, that was a show and wema ni fun kama wengine wote. I don’t think kama by not picking Wema’s money you are proving a point to Jokate. Wanasemage “what goes around, comes around” Jokate anatakiwa kuwa mwangalifu sana kwa mwanaume kama huyu, by doing that, it only shows that he still have very high feeling for Wema.
   Wema baby, take it easy and just subiri coz am telling you, their days are numbers. Wewe ni mzuri sana and Diamond should really appreciate you, at list for what you did for him, yeye ndio aliyeanza kutoka na Jokate so alikua anategemea wewe kwenye hasiri utamsifia , ooooh pls

   Delete
 5. hongera sana wajina kwa kulitendea hali tukio zima na watu woet waliokuwepo.. nimependa umetoa picha zote na za kila aina na matukio.. Keep it up wajina..

  ReplyDelete
 6. na ww acha kutetea ujinga alieanza kumtukana mwenzie nani km co diamond kuanza kumdhalilisha ndo wema akajibu mapigo acheni kumfanya mdada wa watu km chambo yy almas ndo kisa ya yote hayo,dada wa watu alimpenda kwa moyo wote na watu wakaanza kusema lkn hakujal kitu alibaki na msimamo wake wa kuwa na hy almas mwisho wa siku ndo hayo yamemkuta,pole wema ndo yaduania hayo...!

  ReplyDelete
 7. wakati mwingine kukosa shule kunachangia hata ukiwa super star utachemsha tu almasi amechemsha vibaya na wema alitakiwa asiende kabisa unategemea nini kwa mwanaume wa kibongo mtoto wa uswahilini, muuza mitumba na katoka kama bahati tu please wema jifunze uskubali kuumizwa kila siku, Tafuta vitu vingine vya kufanya.

  ReplyDelete
 8. Wewe unaesema eti Wema alimsema Diamond ana nuksi ni wapi? Mbona sie hayo maneno hatukusikia, kwani Wema keshahojiwa mara kibao lakini hatujamsikia akisema hayo maneno. ITAKUWA NI WEWE WEWE KIPUPLISH UNAYETANGAZA HAYO MANENO KWENYE MAGAZETI YA UDAKU NA KWENYE MABLOGU! Imekula kwako hiyo wanaume mpaka wanawake wastaarabu wenye akili zao timamu hawakufurahia ujinga alioufanya. Sana sana amejiharibia kwa wapiga kura huu sio wakati wa kuwauzi watu huku unategemea wakupigie kura mie simpi kura yangu mtu asiyeheshimu wanawake.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wanawake wa siku hizi bwana mnajirahisisha wenyewe halafu mnataka muheshimiwe. kwa tamaduni na mazoea yetu tuliyoyazoea hasa sisi watanzania mkishaachana na mpenzi wako wengine hata salamu hakuna, sasa wewe wema ulijua kabisa wewe na huyo kijana hamuiv chungu kimoja ulienda pale kufanya nini> umejitakia maana huwa unapenda sana sifa za kijanga ndio ukome mama> hongera sana Diamond, na wewe kama hutampa kura yako ya kwako miye nitampa

   Delete
 9. Ni kweli Diamond kukataa kupokea pesa ya Wema si jambo zuri na vile vile sijaona baya alilolitenda Diamond wala Jokate. Hii ni sawa mke au mume kutoka nje ya ndoa kwa kutafuta afueni/pumziko kutokana ama gubu au tabia chafu ya mmoja wapo. Na vile vile hata siku moja mwanamke hana ubavu wa kushindana na mwanaume, basi hata ndoa zisingedumu mpaka watu wanapata wajukuu kama wanawake tusingekuwa wavumilivu.

  Kiukweli Wema hajatulia na nna uhakika juu ya uzuri wake bt hakuna mwanamme atakaye mtongoza akawa na fikra ya kuwa na future na Wema hakuna ataishiwa kuchezewa tu na alivyokuwa hana akili akipata bwana baada ya kujitengenezea maisha yeye anajinadi bingwa wa kuchukua waume za watu. Angalieni wanaume wote aliokuwa nao hakuna hata mmoja aliyeachana naye bila ya scandle. Namuonea huruma mtoto wa mwanamke mwenzangu.

  Kimsingi kwa sasa tunatakiwa tumshauri tu Wema jinsi ya kuishi na sio kumsifia ujinga mtoto wa watu coz anazidi kuharibikiwa kwa sifa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wanaume wa Kibongo akikuacha ni sherehe lakini ukimuacha ndio kama hayo huwa wanataka kuabudiwa na huu si wakati ule wa kuabudiana wajameni akha! Sisi tunazungumzia tukio la kishenzi alilolifanya huyo Almasi kwani watu mkiachana ndio mfanyiane vitimbi? Mbona hayo mambo hayako uswahilini wajameni, si tunaona zamani walioachana wanakutana shughulini na wanasalimiana kama kawa,na watu wanasema fulani na mtalaka wake wale pale wanaongea. Na tena hao ndio wako kwenye ndoa seuze yeye? aliyemwambia afanye hicho kitendo kamuharibia maana ameshapunguza wapiga kura, aliyepata hasara ni yeye na si Wema.

   Na kuhusu Wema bora yeye wanaume wake wanajulikana kuwa idadi kuliko wengi wetu, tumepururaa weee mpaka tulivyopata wakutuoa tumetulia ni wanawake wachache siku hizi wanaolewa na mwanaume huyo huyo aliyeanza nae. Wengi tunakutana na wanaume wanatudanganya mwisho tunawafumania tunaachana nao au hata bila kufumania mtu unaona tu kuwa huyu hana mwelekeo unamuacha, sasa cha ajabu kwa Wema kuacha hao wanaume kiko wapi? Tena watoto wa siku hizi wanaanza kuwa na boyfriend tangu primary school unakuta tayari amekwishaachana na boyfriend 2 wakati anamaliza la 7. Akienda secondary nako mpaka anamaliza form 4 kishakuwa na boyfriend 2 au hata 3 au 4. Mimi najua kwa sababu nafanya counselling na watoto wa kike, wengi wanakusimulia unashangaa. Kuna wengine wazazi wao wanawasomesha very expensive school lakini wanatembea na vijana wanaouza maduka huko mtaani kwao au shamba boy au hata wale wauza vitu, na shuleni wana boyfriend. Kwa hiyo wakati tunamuonea huruma mtoto wa mwanamke mwenzetu turudi ndani tusema na wakwetu pia kwani hawana tofauti na Wema. Ndio kizazi hiki kilivyo bora Wema yeye yuko muwazi hajifichi kuliko wanayofanya watoto wetu.

   Sina lengo la kumtetea au kusifia yake ila mimi huwa nashangaa sana tunapomnyooshea kidole Wema, pengine hatujui ya watoto wetu ni mazito kuliko ya Wema. Wengine tunawaona kwenye mafacebook watoto wadogo 14, 15, na 16 wanavyogombea wanaume unasema Yarabi tunusuru na visasi vyetu. Na nchi yetu ambavyo wanaume hawana woga kutembea na watoto wadogo ni kazi kweli kweli, tofauti na nchi za wenzetu sheria zilizopo ni kali. Sasa hawa watoto wakikuwa wataolewa na kukaa watulie majumbani mwao kwa sababu ya kwao yako chini ya kapeti.

   Delete
  2. Kwa kweli Anonymous Apr 3, 2012 02:18 PM Umesema ukweli mtupu Wema anahesabika na hao maboyfriend kwa sababu ni popular anajulikana ni rahisi kwa watu na media kujua na kusambaza kwa haraka , ukirudi huku nyuma sis kina hatuonekani wala hatujulikani ukihesabia mpaka unaogopa hivi ni mimi kweli . So stop talking and judging wema for everything, Wema ni mwanadamu si malaika na hakuna mwanadamu aliyetimia. Take time to review ur boyfriends before counting

   Delete
 10. jamani jamani jamani nyie acheni uswahili wenu kwani kura za Diamond zinahusiana nini na ugomvi wao na Wema? acheni hizo bwana, mtu anapewa kura kwa kazi zake sio maugomvi yao, sisi yanatuhusu nini acheni hizo mimi kura zangu atazipata nyingi tu, mambo ya ugomvi wao hayatuhusu. acheni hizooo! Wema mwenyewe keshampa kura nyingi tu!!!!

  ReplyDelete
 11. Diamond Keepit up! wasikukatishe tamaa mzee kaza buti, yote hayo ni vijimambo vya ujana tu, ulimpenda Wema zamu yake imeisha songa Mbele, Umepata kura zangu Mazee. Wema usijali wala usisononeke hayo mambo madogo sana na wewe pia mrembo sana Wengi wanameza mate hayo yaliyotokea ni sehemu ya mitihani ya Mapenzi, wako wa dhati yuko njiani.

  ReplyDelete
 12. hayo yote yaliyotokea ni kwamba Diamond bado anamfeel Wema nyie hamuoni jamani? We mdogo wangu Diamond mrudie binti kama bado yupo moyoni, hukupashwa kuonyesha umma ushamba ulioufanya, Wema kama mimi ni wewe wala nisingeenda kwenye ile shaw,kwa kuwa mambo ya hawa wananume hayaeleweki kabisa sasa kama hivyo kakuabisha huoni? Lakini ujue kuwa huo sio mwisho wa maisha songa mbele,kwanza wewe mrembo sana Wema hata Jokate hakupati hata kisigino, usijali mamy!

  ReplyDelete