MAULID YA MTUME MUHAMMAD (S.W.A) MADRASSATUL UKWAMA-MAGOMENI

Umoja wa kina mama wa kiislam Mkurumla (UKWAMA) Walisoma Maulid ya Mtume siku ya Jumapili Mashughuli Blog ilikuwa pamoja nao 

Bonyeza kitufe usikie kaswida toka madrasa Istwam toka Temeke

Wanawake Wakisoma milango ya maulid
Huyu ni mmojawapo wa watoto Yatima, akisoma utenzi wa kumsifu Mtume Muhamad (S.W.A) mashallah! watoto yatima hawa wanalelewa mtaa wa msanga magomeni, kitaka kuwasaidia chochote ulicho nacho wasiliana na Mashughuli Blog - 0655 426100, shime tuwasaidieni mayatima tupate thawabu zetu!!!

MC wa shughuli hiyo akiongoza

Bismillah      Rahman     Rahim

Risala Fupi ya Madrasa ya Umoja wa Kinamama wa Kiislam Makurumla (UKWAMA)

Madrassa ina umri wa miaka mine (4) toka ianzishwe, Ilianza na wanafunzi 65 kutokana na umri wengine wapo nyumbani mpaka sasa wanahudhuria ni wanafunzi 45.
Waliohitimu masomo ya mwanzo Juzuu Amma ni wanafunzi 20 na 25 waliobakia maendeleo yao yanaridhisha.

Kila mwanamama wa Makurumla na mitaa inayozunguka Makurumla na wanakaribishwa katika madrasa hii.

Lengo na dhumuni la madrasa ni kuwakumbisha waliosahau na kuawafundisha wasio jua kabisa na kumjua Mwenyezi Mungu na Mtume wake Muhamad (S.W.A).

Pia tunapenda kuwa shukuu wote mlio hudhuria kutuunga mkono hakuna cha kuwalipa isipokuwa M/Mungu.

Piga no ya simu +255 713 402 892 hii kama unataka kujua zaidi kuhusu madrasa!

KARIBUNI SANA!!

Bi Amina akiangalia kama mambo yanakwenda sawa, hongera mama yangu jaza yako iko kwa mola!

wanafunzi toka madrasa istwam toka Temeke wakiimba kaswida nzuri sana!!


Mama huyu akiimba utenzi wa kusifu Maulid kwa mbwembwe zote na watu wakimtunza kwa furahaHajaat Salma na Maalim wa Madrasat Ukwama akifurahia Maulid ya Mtume Muhamad (S.W.A)
 Mirashi na Udi vikipitishwa baada ya kusimama kiam!

Hajaat Salma akiimba kaswida kwa furahaShamimu, kweli milima haikutani lakini binadamu hukutana! long time eeh! hongera na sasa mama wa totoz 2


Barka ikitayarishwa, ukila chakula cha kwenye shughuli kama hii basi utapata barka!, wakati mie naondoka baada ya kula barka na watu wengine wakitayarishiwa, Namshukuru Bi Amina ndiye alikuyekuwa mwenyeji wangu nilipokelewa vinzuri sana!! inshaalah tukutane mwakani tukijaaliwa uhai na M\MUNGU na Maulid yawe makubwa zaidi!!!


Post a Comment

4 Comments

 1. Imependeza, Jazakallah aghira

  Mrs. Mbarouk

  ReplyDelete
 2. MaashaALLAH, maulid yalikuwa mazuri sana na watu wote wamependeza, Bi Amina na Bi Salma(Mama shughuli) mwenyezimungu akupeni uhai na afya njema ili mwakani tupate maulid kubwa zaidi.
  Allah Hafidh

  Mama Tawadud

  ReplyDelete
 3. amin rabil allamin kweli mauli yalikuwa mazuri mungu awape imri mrefu

  ReplyDelete