TANT BOY AMFANYIA HAULI MWANAYE MAREHEMU JAFFARI


 

BONYEZA KITUFE KUANGALIA KIDEO


 
Bi Mwana anaishi kigamboni nimeshawahi kukutana naye kama mara 2/3 hivi lakinia ana mawaidha mazuri sana! Hapa akisoma utezi alioundaa kwa ajili ya historia ya marehemu Jaffari sote tulilia jamani na mie sie mchoyo nimewaletea utezi wake huu hapa ukimuhitaji kwa shughuli yoyote ile piga simu no.: 0653-766306/0777-766306
Utenzi
Baada ya kuwasalimia

Mbele ninaendelea
Nawapa historia
Ya marehemu sikia

Kumtaja sinabudi
Marehemu Jaffar
Amrehemu wadudi
Dua tunamuombea

Naanza kuielezea
Mwaka aliozaliwa
Mpaka alijifia
Mupate kuitambua

Tarehe kumi na tatu
Mwezi wa kumi na mbili
Mwaka tisini na tatu
Ndipo alipozaliwa

Kisha akaendelea
Masomo akapatiwa
Na shule tawatajia
Zote alizosomea

Kaanza darasa la awali
Katika shule ya muhimbili
Hadi la tano jamani
Shule akahamishwa

Darasa la 6 kahamishwa
Shule ya Ilala boma
Na hapo pia kasoma
Miezi mitano pia

Tarehe saba kwa kweli
Akaipata ajali
Na aligongwa na gari
Na hapo ikamuuwa

Inaendelea...! hapa nilipenda kuonyesha jinsi anavyotunga mashairi lakini ni beti ni nyingi sana


 
Tant Boy pole dada kazi ya Mungu haina makosa

Dida yuko na somo pamoja


Wanaume walikaa ndani wachache ndugu wa familia

Moody Madenge kanzu ya ukwee'e


Chakula by Miriam Twahir kama kawa


 
baada ya shibe...!!!
 
 
  

Post a Comment

2 Comments

 1. Assaallaam Allleykum Mashughuli
  Nashukuru sana sana yaani unavyotupostia hizi video,,yaani we acha tu!Sijui nikushukuruje,,,Nimependa sauti ya huyo dada,,yaani nimejihisi niko Peponi tayali!,,,Nilikuwa niandike kukuuliza namba zake au Email yake ,,kumbe baadae nikakuta umeisha iweka,,,Ni kweli wewe sio mchoyo,,huna 'roho ya kwa nini',,,Leo imebidi nikujulishe kuwa Video zote unazotuma mimi zinanipa faraja sana.na ile iliyopita ingawa namba za wale waliokuwa wanaimba Qasidah katika Maulid ya Mazao ya Mtume hukuweka simu zao.
  Shukran mno mno!
  JazzakAllah Khairan
  Ahlam,,,London!

  ReplyDelete
 2. Kwani mkorogo bongo ni free sioni mwenye rangi yake halisi ,mtumeeeeee!!!!

  ReplyDelete