ISOME HAPA CHANZO CHA KIFO CHA KANUMBA LULU AU ELIZABETH MICHAEL HAKUKIMBIA JAMANI!!! WALIKWENDA PAMOJA NA SETH POLISI OSTERBAY KUCHUKUA PF3 NDIPO POLISI WAKAMSHIKILIA KUTOKANA NA MAELEZO WALIYOTOA POLISI


MAELFU ya wapenzi wa sanaa ya filamu nchini, alfajiri ya kuamkia jana waliduwaa mithili ya watu waliopigwa sindano ya ganzi baada ya kuenea kwa taarifa za kifo cha ghafla cha msanii namba moja wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba (28).

Taarifa za kifo cha Kanumba zilisambaa kwa kasi mithili ya moto katika nyika kavu na kuikuta alfajiri ya jana, ikigeuka kibarua kigumu kwa idadi kubwa ya watu, kusaka stesheni mbalimbali za redio, televisheni mitandao ya kompyuta huku wengine wakihangaika kupiga simu huku na kule, kutafuta ukweli wa tukio hilo,lililotikisa si Tanzania tu bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Kanumba alifariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi, Kanda ya Kinondoni, Charles Kenyela, ziinaeleza kuwa kifo cha msanii huyo kilitokana na ugomvi uliotokea kati yake na mpenzi wake ndani ya nyumba yake.

Taarifa za kifo cha Kanumba zilianza kusambaa kuanzia saa 10.00 alfajiri na kuenea kwa kasi ambapo hadi kufikia saa moja asubuhi, mamia ya watu walikuwa wamejazana nyumbani Kanumba kutaka kuthibitisha habari hizo.
Kadri muda ulivyozidi kusogea ndivyo idadi ya watu ilizidi kuongezeka nyumbani kwa msaani huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutoka na filamu zake kuuzwa na kuoneshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni, ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa watu waliomiminika kwa haraka nyumbani kwa kanumba jana ni wasanii wa fani mbalimbali nchini,  wanasiasa na viongozi mbalimbali wa Serikali

Chanzo cha kifo chake
Kwa mujibu wa maelezo ya mdogo wake aitwaye Seth ambaye alikuwepo eneo la tukio, alisema kaka yake alishinda nyumbani na baada ya kula chakula cha jioni, alimwambia wajiandae kutoka.
Seth alisema kuwa wakati Kanumba akiwa tayari amejiandaa, walisikia mlio wa gari lifunga breki nje ya nyumba. 
Alisema gari hilo lilikuwa limemleta mpenzi wa kaka yake msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ambaye aliingia ndani na kwenda moja kwa moja chumbani kwa Kanumba.
Baada ya kuingia ndani, muda mfupi alisikia sauti zilizoashiria kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya wapenzi hao.
“Ghafla ulizuka mzozo ndani na dakika chache baadaye, Lulu alitoka na kuja kuniambia kuwa Kanumba amedondoka baada ya kujigonga ukutani na kwamba yupo taabani hajitambui,” alisema Seth.
Alisema alipoingia chumbani, alimkuta kaka yake akiwa katika hali mbaya hivyo akaamua kumpigia simu daktari wake, ambaye alipofika na kuwashauri wampeleke haraka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.
Seth alisema kabla ya kufika Muhimbili  walipitia Kituo cha Polisi cha Oysterbay kupatiwa Fomu ya matibabu (PF3).
Hata hivyo, baada ya polisi kupata maelezo ya awali ya ugomvi huo, walimshikilia Lulu kituoni hapo na kumwacha Seth akimpeleka Kanumba hospitali.
Alisema walipofikia Hospitali ya Muhimbili, madakati waligundua kuwa tayari Kanumba alishaaga dunia.

Kamanda Kenyela
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi uliotokea kati yake na rafiki yake wa kike Lulu.
"Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo (jana) majira ya saa tisa usiku, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ugomvi kati yake na rafiki yake wa kike anayejulikana kwa jina la Elizabeth Michael 'Lulu' mwenye umri wa miaka 18.
Alisema kabla ya ugomvi huo kutokea kati yao wakiwa chumbani, simu ya Lulu iliita na akaamua kutoka nje kupokea kitendo kilichomuudhi Kanumba.
Kamanda Kenyela alisema Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti akitaka aelezwe kwanini alitoka nje kupokea simu huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.
Aliongeza baada ya Lulu kuona Kanumba akimfuata aliamua kukimbia kutoka nje ya geti , lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba  alimkamata na kumrudishwa ndani.
Kamanda Kenyela, alisema Kanumba akiwa amemshikilia waliingia wote chumbani na kufunga mlango. 
Hata hivyo, alisema haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba. 
Kamanda huyo alisema Lulu anaeleza kuwa baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini.
Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Kanumba alikuwa amekunywa Whisky (pombe kali) aina ya Jacky Daniel, hata hivyo, bado wanachunguza zaidi kujua kama kweli Kanumba alilegea tu na kuanguka, ama alipigwa na kitu kizito kichwani au alisukumwa kwa nguvu na kumfanya aangukie kisogo.
“Uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani kwa tuhuma za mauaji,” aliongeza Kamanda Kenyela.

kwa habari zaidi za uhakika na sio maneno yanayozushwa mtaani ingia humu                                                                    


Post a Comment

5 Comments

 1. Duh! Namsikitikia pia huyu msichani. Ni mdogo, na hatakama hakumuua Kanumba, lakini chamoto atakiona. Inawezekana jamaa alikuwa na aneurysm iliyokuwa triggered na kujigonga. Haiwezakani mtu akafa mara moja hivyo. Sijui hata hospitali zetu kama wanajua kucheki vitu kama hivi. I guess tutasubiri majibu ya hospitali. Asante Mashughuli kwa kuendelea kuturushia hizi habari.

  ReplyDelete
 2. Jamani ingia 8020fashions.blogspot.com kuna video ya huyo Seth mdogo wa marehemu akielezea tukio na kwa maneno yake akasema alienda kumfuata daktari na kurudi nyumbani Lulu hakuwepo! SO watch the video!

  ReplyDelete
 3. mmg mi bado tu nasikitika!! pamoja na hayo sheria ya nchi yetu is not good ukija kwenye maswla ya afya. mtu yuko mahututi au amepata ajali wherever it is eti mpaka ulete pf3 ndo upate matibabu instead of starting service ndo pf3 ifate hata kama mtu alikuwa hfi atakufa kwa ajili ya stupid law.may be wasinge enda police kwanza wangemwahi.

  ReplyDelete
 4. Jamani ni nasikitika tu coz sijui haya maelezo kayatoa nani, Naomba kurekebisha hapo kuwa kabla ya kwenda hospitali walienda polisi ukweli ni kwamba seth alikwenda polisi akitokea muhimbili baada ya kanumba kudhibitishwa ameshakufa hivyo wahifadhi maiti walihitaji PF3 ili wahifadhi maiti ya kanumba, na wala Lulu hakuambatana na seth kwenda polisi Lulu alikimbia palepale nyumbani baada ya seth kumuacha amuangalie Kanumba akidhani kuwa alizimia na seth ndio alitoka kumfuata dr, na pia kanumba na lulu hawakufukazana kama ilivyoripotiwa hapo baada ya Lulu kuingia chumbani wala hawakutoka mpaka lulu alipopiga kelele kumuita seth!kwanini watu wasinyooshe maelezo ili sheria ichukue mkondo wake.........R.I.P Kanumba

  ReplyDelete
 5. pole mama kanumba
  sisi watanzania tuaoishi Cambodia tunatoa mkono wa pole

  ReplyDelete