ZIANA KITCHEN PARTY

BRIDE           ::ZIANA
VENUE          ::MANGO HALL
COLOR          ::TANGERINE & GREEN
MC                 ::DALILA JAGAR - +255 713 265 137
CATERER      ::TALMA CATERER


 Ziana akiwa na masomo wake baada ya kuingia ukumbini


 Mariam Twahir akikaribisha wageni waalikwa...!!! ndani ya bazee original red
 Zawadi


 Mambo yanaenda yakiongezeka, sasa nazo zagatolewa kwenye k-party
   


Somo akikabidhi kabati, viombo vingine naona vilichelewa kufika ukumbini wakashindwa kupanga
 Masomo na black color, nakuona Halima Mfinanga...!!

 
  Mashosti walicheza kwaito....kwanza

 Huyu ndio mpishi mkuu wa Talma Cateree!!, ukiona chakula kitamu basi bi dada huyu ndie anatupikia akienda kutoa zawadi kwa bi harusi wake!!!!!
   alikabidhi coffee table
  
Aunty Samia akienda kutoa zawadi kwa niaba ankal Immu, wamjua ankal Imuu wewe!!!
 
Aunty Samia na kampani yake!!!!

 Mkuregenzi wa Talma Catter , Mariam Twahir akimpeka Ziana kuona zawadi yake!!

Mariam Twahir na kampani yake walitoa zawadi ya sofa 

CHAMBUA CHAMBUA
si unajua inaingia kati ya shughuli!!!
Kwanza kabisa wadau ningependa kupata neno ambalo MC wengi wanalitumia, japokuwa neno hilo limetokana na kizungu lakini mie sipati jibu bado, wakati mtu anatoa zawadi au kutunza huwa na mashostito wake wanaomsindikiza sasa wenyewe wanaita kampani yake, does it stand for company?? or !!! plse help!! kwa yoyote anayejua

Pishi
By TALMA Caterer 

Burdaaaani.....!!!


NYUSO


Swaga
Post a Comment

20 Comments

 1. Hongera bi Arusi mtarajiwa, amependeza hana makorokoro meengi.Swali; Hawa wanaume wamefuata nini hapo?

  ReplyDelete
 2. Bi harusi umependeza sana, ila jamani wageni waalikwa hizi make ups huwa mnapakwa wapi jamani? kha mpk nimesikia kichefuchefu.

  ReplyDelete
 3. hahahaha bi rachel unauliza jibu shoti haaaaaaaaaaaaaaaa halllaaaaaaaaaaa nimeipenda rangi ya shughuli bi mtarajiwa kapendeza sana

  ReplyDelete
 4. mikorogo jaman khaaaaaaa wanawake wa dar too much yani nasikia kutapika wengine wanene wamepasuka mikono sijui ni unene make up mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 5. kweli bi harusi mcute kapendza sana, na kuna badhi ya watu wamependeza yani make up imetulia...ila hao wengine jamani hivi hamjioni mnavopakwa mnakuwa kama mmewekwa frijini......mama wa blogu hebu wasaidie pale unapowapiga pcha waambie wapunguze hayo marangi jamani wanatia kichefuchefu yani inaonyesha ni ushamba wa hali ya juu ..kujisiliba gani huko....mikorogo tuuu!!! fyuuuu!

  ReplyDelete
  Replies
  1. B harusi kapendeza sana Mashaalwah mamy hongera sana. Langu kwa wageni Waalikwa jamani hizi Make ups jamani embu tujiangalie kabla hatujatoka majumbani maana zinatisha. Kila la kheri B harusi

   Delete
 6. nimempenda kwali huyu binti jamani, nakaonea hata huruma kwa kuja huku kwenye mijanaume iliyokosa aibu karne hii. uwe mvumilivu mwanangu, heshima na busara vitumike zaidi kwenye ndoa yako, utulie kama sura yako! nakutakia maisha mazuri yenye furaha na amani! mama nahia.

  ReplyDelete
 7. yap mashughuli,wanaitwa companions ndio watu wanaomsindikiza mwingine

  ReplyDelete
 8. Teh tehtheteh@da'Lulu mimi sielewi,kwani kuna wapiga picha,Mc,Ma Dj na mambo mengi ya hapo yaweza kufanywa na wanawake wenyewe.Na tukiaga nyumbani twaenda K/p baba ngina anabaki home kwani ni Wanawake tuu huko,sasa akiona picha anakuta wanaume pia wapo!!hahahahahha ngoja niishie hapa.Hii nitaifanya mada pale kwangu.

  ReplyDelete
 9. Bi Harusi Ma'ansha'Allah kapendeza mno simple but bomba!!!Hizo Make up mtu hawezi kukuelewa ukimwambia punguza,,ila baadae akienda kujichanganya na wastaarabu ndo atagundua kuwa yeye amekuwa kama kiroja,au sanamu,
  na katika picha inaonekana kama mtu kaganda uso umefreeze yaani we acha tu,,
  Kuhusu hilo swali lako mama Mashughuli,,Kwetu tumezoea sana company lakini kiukweli kabisa ni companions,,yaani watu wanao kupa tough,au wapambe,wasindikizaji,,ukitafsiri kwa kiswahili inakuja kama maana ya kusema company lakini sio!!!Hilo neno tunaliweka pahala sio,,,Naona aliyelizoesha mwanzo hakutamka mpaka mwisho sisi tukafikiri ni KAMPANI KUMBE NI KAMPANIONI

  AHSANTE MASHUGHULI KWA KAZI YAKO NZURI MNO!
  NIMEONA BLOG NYINGI LAKINI YA KUNIRUDISHA HOME,,WEWE HUNA MPINZANI MA'ANSHA'ALLAH

  AHLAM,,,LONDON

  ReplyDelete
 10. Bi Harusi kapendeza sana mashallah! Ila hao wengine wanatunza masofa na cofee table wao wenyewe wanavyo? Au kujionesha tu. Hahahahahaha!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Usicheze na hao Wamama wa mujini, wanapesa kama nini hao, mie siwajui kihivyo lakini ninawaona kwenye shughuli za mashughuli. Kwa mfano huyo mama aliyetunza masofa ana catering business na shughuli nyingi za humu naona mpishi ni yeye. Pengine ukute ana nyumba Kariakoo, wee achana na hawa malordlady wakianza kutunzana pesa utakimbia!

   Delete
 11. Chambua chambua yangu, ukumbi umeharibu shughuli ya watu, bi kharusi kapendeza mashallah lakini sakafu ya ukumbini utafikiri haina mwenyewe. Wewe mwenye ukumbi unapokea pesa za watu kisha hiyo sakafu inakushinda kutengeneza?

  ReplyDelete
 12. Huyo msichana alivyo mzuri mashallah, ukichanganya na hilo jopo la masomo wa ukwee mbona huyo mume atafaidi. Na akitoka nje ya ndoa yake basi atakuwa wa ajabu huyo mwanaume!

  ReplyDelete
 13. jamany bi.harusi kapendeza mashallah ila hao wageni waalikwa jamany hayo ma make-up wanatisha na mikorogo miili yao kuanzia sura mpaka migii mama yangu haitamaniki ...waambie wapunguze kwani black is beauty

  ReplyDelete
 14. Namjibu anonymous wa tarehe 5may, hao wa mama wa mini wanapenda tu kujionesha na kujidai kutunza wengine hata nyumba na pa kukaa hawana kuweni na maendeleo ya maana kwanza jamani wapo tayari wawe na madeni ilimradi waonekane kwenye ma internet.

  ReplyDelete
 15. JAMANI BI HARUSI KAPENDEZA SANAAAAAAAAAAA MASHAALLAH, ILA HAO WAGENI, NDUGU ZAKE NA MAJIRANI AIBU TUPU, HIZO MAKEUPS JAMANI MKIWA MNATOKA MUWAULIZE WAUME ZENU, MAHOUSEGIRL NA NDUGU JAMANI NI AIBU, MNATAFUTA NINI WANAWAKE WENZANGU? UMRI UMESHA KWENDA NGUO FUPI ZA NINI NA MINYAMA YA UZEENI? MUWAACHIE WA 18TH JAMANI WATOTO WENU, YAANI WENGINE WAMEONEKANA KAMA WANATOKA KUCHEZA NGOMA, MTUMEEEEEEEEEE YAANI NIMECHEKA HAPA, SIPATI KUSEMA, NI AIBU NA WALA HAMPENDEZI KABISA MNAJIDANGANYA, NA HAO WAUME HAMNA WA KUWAANGALIA MKIWA MNATOKA JAMANI, NA HAO WANAOTUNZA HAYO MAKOCHI NA MAFENICHA NI KWELI MAKWAO HAWANA WANAKALIA MIKEKA, DUUUUUUH NI AIBU KWELI KWELI JAMANI WANAWAKE WENZANGU, USHAURI WANGU MKIWA MNAKWENDA HARUSI MAKEUP KWA MBALIIIIIIIIII UTAPENDEZA TU SIO KUJIKANDIKA JAMANI

  ReplyDelete
 16. HARUSI NZURI ILA WANAWAKE MAKEUPS MMEJIABISHA DADA ZANGU

  ReplyDelete
 17. BI HARUSI HONGERA NA UMEPENDEZA ILA MIMI DADA YAKO NAKUONEA HURUMA HUKU UNAKOKWENDA, MAANA HAWA WANAUME HAWATOSHEKI, KILA WAMUONAE WANAMUONA NI MZURI KULIKO WEWE, NA HIZI NDOA ZA SIKU HIZI HAZINA CHA UISLAMU WA UKRISTU NDOA ZOTE SIKU HIZI WANAWAKE WATATU WATATU BIBI WEEEE, POLE ILA UKITAKA KUKAA KWENYE NDOA YAKO, KUWA MVUMILIVU, MPENDE MUMEO, USISIKILIZE MANENO YA WATU, KUWA MNYENYEKEVU NDIO DAWA KWA WANAUME, UKIJITIA VUVUZELA ATAKUBWAGA, SIO KUKUACHA, ATAKUWA NA WEWE ILA ATAONGEZA MWINGINE, WEWE UTAKAA TU NDANI KAMA MKE WA KWANZA KWA AJILI YA KULEA HAO WATOTO, NA WANAJUA KWELI KUDANGANYA, ATAJIFANYA ANAKUPENDA NDIO MAANA YUPO NA WEWE KUMBE HAKUNA LOLOTE ANAPENDWA HUYO WA PILI NA WATATU, WEWE TENA LEA WATOTO WAKO, MAPENZI TENA HAKUNA, PUNGUZA DOMO NA KUWA MNYENYEKEVU KWA MUMEO

  ReplyDelete
 18. What your saying is completely genuine. I recognize that everyone should say the exact same issue, conversely I just
  think that you place it in a approach that absolutely everyone can recognize.
  I also actually for example the photos you set in right here.
  That they in shape so nicely with what youre attempting to say.
  Im sure youll achieve so quite a large amount of folks with what youve obtained to say.


  Feel free to surf to my web blog :: background check reviews

  ReplyDelete