TAMAA!!!

WADAU NIMESOMA HII STORY KWA FB FRIEND WANGU SITOPENDA KUTAJA JINA LAKE BILA RIDHAA YAKE, INAFUNDISHA, NIMEAMUA KUSHARE NA NYIE...!!!
Anachokifanya anti hapo pichani, si kigeni, anatengeneza chapati. Anti huyu huamka saa kumna1 asbuhi, akoke moto, akande unga, atengeneze chapati, akaange. Hii ni kazi yake ya kila siku. Anti huyu amekuwa akipika chapati miaka mi5 sasa, hivyo hivyo akiziuza kwa shida, maana kinachofuatia hapo ni kusubiri wateja, chapati moja TSH 200/=. Bahati, hapo jirani yake akahamia mdada mmoja, akawa mteja wake, anachukua chapati mbili kila siku anaenda nazo kazini. Mara yule mdada akaanza chukua nne, mara 8 mara 10, mara
akaweka oda ya chapati 100 kila siku. Mama akawa hana jasho la kuuza tena, yaani dada wa watu akifika tu analamba chapati 100 anasepa. Kwa vile anachukua 100, mdada akaomba awe anauziwa moja kwa 150/=, anti akaona inalipa, anti akakubali, mdada sasa akawa anachukua chapati 200 kila siku. Mama wa watu akaanza fuatilia kisirisiri, mdada anapeleka wapi? Kumbe yule dada anazichukua, anaenda nunua foil, anazifunga kwenye foil anauza Ofisini kwao na ofisi ya shosti yake jirani. Anauza moja Mia Tano. Mama kugundua, kaanza vimba, mara ananuna nuna, mara siku nyingine atengeneze 40 tu, mara aseme leo nnaumwa, mara leo nna oda kubwa dadaangu siwezi kukupa, basi akendelea hivyo ili mdada ashindwe. Mdada akamwambia anti naona mie niache tu. Anti akafurahi. Kesho yake anti akatengeneza 200 akamtuma mtoto wake wa kike akaziuze ktk zile ofisi mbili, unajua nini, aliuza 10 tu. Yule mdada alishaangaliaga plan B, anachukua kwa mama mwingine, tena anazipata kwa mia mia, sasa ana ofisi ya 3 anasaplai chapati 300 kila asbuhi. Kwa huyu mama mwingine jiko halikuwa zuri akampa jiko zuri na hotpots.

LIKE OUR  FACEBOOK PAGE , FOLLOW MASHUGHULIBLOG ON INSTAGRAM & TWITTER
Tujifunze:

1. Ukiuza Samsung yako laki, aliyenunua akaenda uza milioni, piga kimya, haikuhusu!

2. Ukiona mwenzako anauza sana, usidhanie basi nawe unaweza anza chako ka kile ukauza sana, hujui siri ya biashara yake

3. Anti angetakiwa afurahie mafanikio ya mdada, fursa ya huyu anti ni kuomba masalahi, walau sasa aombe dada anunue kwa shs 170, ajenge hoja na sio kumfanyia visa.
4, HUYU MDADA ANANUNUA FOIL KUFUNGA CHAPATI
6. Endeleeni wenyewe....7.... 8..... 9.....
UKIENDELEZA NAOMBA TUMA COMMENT SOTE TUSOME

MIMI MASHUGHULI NIMEPENDA 'PLAN B' YA MDADA SIKU ZOTE UKIWA UNAFANYA KITU LAZIMA UWE NA 'PLAN B' PEMBENI

Post a Comment

15 Comments

 1. 7. Analipa nauli kama hana usafiri binafsi ambao pia inabidi aweke mafuta.

  ReplyDelete
 2. kuenda kwenye hizo ofisi nyingine kutafuta wateja au kama anatumia simu yake kuwajulisha.

  ReplyDelete
 3. 8. Kule ofisini mdada anakopwa hizo chapati analipwa mwisho wa mwezi, na wengine wanamrusha kabisa hawalipi.

  ReplyDelete
 4. huyu mdada wateja wake wamaofisini wameshamzoea na kumuamini na pia kupenda wanachokinunua kwake (chapati) ni vigumu kuweza kuwa na uhusiano wa kibiashara kwa siku moja kwa wateja wengi kama alivyotegemea huyu mdada

  ReplyDelete
 5. Watu hatuelewi kabisa, ni bora upate faida kidogo kidogo lakini unaipata kila siku, kuleko alivyodhani atapata faida kubwa kumbe hakupata kabisa. Kila mtu na riziki yake na kila mtu na mvuto wake hilo utake usitake lipo. Huyu wa kwanza samahani lakini ni mjinga na huyu wa pili ni mwerevu. Tumejifunza.

  ReplyDelete
 6. Sasa huyo muuza chapati anayasoma haya au ndo sisi kufurahisha nafsi zetu?

  ReplyDelete
 7. na pia personality ya huyo mdada wa ofisini inauza

  ReplyDelete
 8. Nadhani ni bora labda angeendelea kumuuzia dada wa ofisini. Faida ya fasta ina shida. Mvumilivu hula mbivu.

  ReplyDelete
 9. Yaani huyo mama muuza chapati mjinga sana. yaani wivu na ubinafsi ndio umempoza. pole yake. hawa ndio watu wasion na maendeleo kabisa

  ReplyDelete
 10. Hivi we mdau unaeuliza kama huyo muuza chapati anayasoma haha unaakili sawasawa kweli? Kesho we uliyeingia huku na kuconment Ni muuza chapati, huoni kwamba watu watajifunza huku kupitia huyo muuza chapati? Nawewe akili yako Ni kama huyo muuza chapati. Unatabia ngumu kama jiwe.

  ReplyDelete
  Replies
  1. I say, na wewe km huyo mama mnunua chapati vile... mana povu linakutoka! Mi nmejifunza kutokula jasho la mwengine!

   Delete
 11. Kwenden zenu wezi wakubwa km huyo mama wa ofsini bas 150 kwa mia 500? Mnyonyaji tu huyo mama anataka kuchuma kwa kutumia nguvu za mwenzie hv mnajua anaumia vp kukanda kila siku chapati huyo mama? Bas at least angeendelea kunnua bei ile ile ya 200 nngemuona wa mana lkn kumlalia kabisa half mnakaa kutetea ujinga hapa ndo mana watu hawaendelei kw sbb ya wanyonyaji km hawa! I wish baba nyerere angekuwa hai akaja mchapa bakora huyo mama. Halaf na ww Helen uibanie hii sitokuelewaa!

  ReplyDelete
  Replies
  1. da shosti, pamoja na darasa lote hilo hujaelewa? ama kweli wanawake na maendeleo TUTASUBIRI SANA. KAMA VIPI BASI DADA WA OFISINI AMEMWACHIA CHAPATI ZAKE. mana mdau unaongea utadhani huyo anayeenda kuuza ofisini hatumii hata garama. mkkanga chapati hapa anafananishwa na mukila anayezalisha shambani, dada wa kuuza ofisini ni mchuuzi....unadhani kuna asiyevuja jasho hapo.....KAKOJOE ULALE BIBIE.akili yako nzito kama uji wa ulezi wa jana

   Delete
  2. Katika maisha haya usiangalie sana unachokipoteza, angalia nini unakipata na uchukue tahadhari ya vitendo vyako usije ukakosa hata hicho kidogo unachokipata kwa kutamani vikubwa ambavyo sio riziki yako.

   Delete
 12. ni kweli kama yeye aliona wa ofisini anapata faida basi angemwambia hata kuwa vitu vimepanda bei ili amuuzie kwa sh.200,ina maana nyie mnaosema kuwa wa ofisini anamlangua mpishi ina maana hamjawahi kufanya biashara???mnachukua bidhaa kwa bei ya chini mnauza twice na wengine hata mara tatu ya bei aliyochukulia sa kwa nini usimuuzie kwa bei uliyochukulia kariakoo,hebu acheni viroho vyenu vya korosho!!!

  ReplyDelete