ANGALIZO-PODA ZA KINA MAMA SHUGHULINI!!!!

LEO NAOMBA KUONGELEA POWDER  SIE WANAWAKE TUNAPAKA USONI ILI TUPENDEZE ZAIDI, NA NITAONGELEA HAPA HAPA KWETU HUSUSANI SHUGHULI NINAZOPOST HAPA KWENYE BLOG, IMEKUWA NI TATIZO SANA KWANGU NINAPOKUTANA NA MTU AMBAYE KAPAKA PODA HAIENDANI NA RANGI YA USO WAKE, KUMWAMBIA NASHINDWA, PICHA HAZIPENDEZI NA SI LENGO LA MASHUGHULIBLOG KUMTOA MTU PICHA YAKE HAIJAPNDEZA ILA PALE NINAPOZIDIWA BASI INABIDI NIFUTE PICHA, UKIJA KWA WATARAJIWA EBU JARIBUNI KUFANYA UCHUNGUZI WAPI UTAREMBWA VINZURI UPENDEZE AU HATA IKIWEZEKANA BEBA PODA ZAKO NENDA NAZO SALOON, KUNA WATU WANAFANYA BIASHARA HAWAJALI KAMA UMEPENDEZA WAO ILIMARADI KAINGIZA PESA, KWANINI UFANYIWE MAKEUP MBAYA KWA BEI ILE ILE UNGEFANYIWA VINZURI??? UNASIKIAJE RAHA USO WAKE UKIPENDEZA?? SWALI NAWAACHIA NYIE WADAU MNISAIDIE TAFADHALI NAOMBA MSITAJE JINA LA MTU YOYOTE YULE  KUTOA MFANO LABDA KWA NIA NJEMA TU..!!! ILA MASHUGHULIBLOG TUMECHOKA NA PODA MBAYA KUANZIA SASA UKIONA PICHA YAKO HAIJATOKA KWENYE BLOG ASILIMIA KUBWA ITAKUWA NI PODA YAKO...!!!

Post a Comment

8 Comments

 1. Hahahahaaaaaaaaaaaaa du umeua ant hellen, kwazi kwenu asikwambie ukipendeza smile huja yenyewe,

  ReplyDelete
 2. Kwa hilo nakusupport asilimia mia moja. Ni kweli kabisa, nadhani ni make up ya uso kwa ujumla ukweli nyingine mh mh tena pale mtu anapotaka ku match na rangi ya shughuli hali ndo inazidi kuwa mbaya maana huko kwenye macho kunakuwa hatari tupu. Hongera kwa hili.

  ReplyDelete
 3. Mtu mweusi tiiii anapaka poda ya mtu mweupe hatareeeee

  ReplyDelete
 4. teh teh teh mada imenikosha waelimishwe mpk kieleweke

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ni ukweli utabaki palepale ninyi akina dada mmezidi manake unapaka makeup hovyohovyo,kwanza angalia rangi yako kwanza utajua unatakiwa ufanye nini c kwa sababu fulani kapaka hivi nawe unakurupuka upake hivyo matokeo yake unakuwa kichekesho kwenye hiyo shughuli,kuna watu nimewafuatilia humu hasa hawa wamama watu wazima kwa kweli watia aibu,badilikeni jamani

   Delete
 5. Hivi ukipaka poda ya aina yako unajisikiaje ukipendeza?, yaan smile huja yenyewe then pia unakuwa unajiamin, na hayo marangi basi ya usoni usikoleze SANA jamani wamama na wadada mbOna ukipaka ya mbali wapendeza tuu. Tubadilike, Mwanamke kupendeza, mwanamke kujipara.

  ReplyDelete
 6. asante sana dada hellen kwakweli co poda tu au eyeshadow lazima tujue tunapaka nini na ngozi zetu ni zipi mana utapakwa make up asubuhi unaamka na chunusi kumbe sio ya ngozi yako na sisi wadada tupunguze mikorogo sasa kwasababu hata ukipakwa make up ngozi yako haikubali asante sana dada kwa kuliona hilo ukiona mengine please yaweke hadharani tena na mifano zaidi zidi kutuelimisha dada

  ReplyDelete
 7. mi huwa na comment kila siku. .watu mfunguke. .mjiangalie sio kila kinachompendeza wema sepetu kitampendeza shamsa ford..Two different things. Angalia rangi yako na kama ni make up hata kama huna uwezo wakununua expensive basi Nenda tuu maduka expensive uulizie skin type yako na make up gani itakupendeza. maana utaishia kujichukia na kupoteza confidence wakati you are beautiful more than the injustice u do on ur face.
  nb
  I love ur blog mdada n love you too.
  mdau
  USA

  ReplyDelete