Home Shopping Center (HSC) yamzawadia mshindi wa ‘Give a Way’!!

KAMPUNI ya uuzaji wa bidhaa za majumbani na ofisini ya Home Shopping Centre (HSC) imemzawadia mshindi wake wa kwanza wa ‘pendezesha nyumba na HSC’,Rehane Jaffer hundi ya sh 500,000. Shindano hilo linaendeshwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na limepewa jina la ‘Give a Way’.
Hundi hiyo ilikabidhiwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Mauzo na Masoko wa HSC, Nadhir Mubarak Bahayan ambaye aliwataka watanzania kushiriki shindano hilo ambalo kila Ijumaa
watakuwa wakijishindia sh. 500,000. “Wateja wetu wa HSC, wanatakiwa kujiunga kwenye
mtandao wetu wa facebook na kisha kututumia picha walizopamba ndani ya nyumba zao zitokanazo
na bidhaa zetu,” alisema Nadhir. Alisema shindano hilo litaendeshwa
kwa mwezi mzima wa Machi. Mshindi huyo aliipongeza
HSC kwa shindano hio na kusema ni faraja kwake na familia yake.
Aidha zoezi hilo ambalo litaendeshwa kwa  muda wa mwezi mzima wa Machi
huku kila Ijumaa ikitarajiwa kutangaza washindi na kukabidhiwa hundi
siku inayofuata.


Post a Comment

0 Comments