HONGERA MBUNIFU ASYIA IDAROUS AWIKA NA MAVAZI YA UBUNIFU NCHINI NAIGERIA!!!

Familia za watanzania wanaoishi nchini Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwa balozi, Balozi Ole Njoolay,  Abuja Nigeria. FOLLOW US ON INSTAGRAM:: MASHUGHULIBLOG
Na Andrew Chale
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni mwa wiki aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho  kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum kwa  ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.
Onyesho hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya Kimataifa ya Nyota  tano ya Sheraton Abuja, usiku wa  April 25,  huku likiudhuriwa na watu wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa kigeni walioongozwa na balozi anayewaiwakilisha  Tanzania, nchini humo Balozi Daniel Ole Njoolay.
Akizungumza na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria,  Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, aliwashukuru watanzania kwa kuandaa onyesho hilo maalum,  kwani limeweza kuitangaza Tanzania kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.
"Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu Wanaigeria wamevutika na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye mavazi ya ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka ya wamasai kutoka  Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia wa Nigeria na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.
Sherehe hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia mabalozi mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye onyesho hilo.  Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy Mapunda, Fatma Mwinyi, Salma Maulid  na wengine wengi.
 “Utanzania wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na kuudumisha  ndani na nje ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao ‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.
 Nigeria ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija  na hata Taifa hilo kuwa juu kiuchumi. 

Post a Comment

2 Comments

  1. hongereni sana sana watanzania wenzetu wa Nigeria

    ReplyDelete
  2. hongereni sana wenzetu mnaoishi nmbali na kukumbuka nyumbani mungu awasaidie

    ReplyDelete