TANGAZO LA KIFO - AMINA-ZAHARA SHABANI MTENGETI

Hajat Mwantumu Shabani Mtengeti (Mwantumu Malale) wa mtaa wa Mlingotini Close, 
Dar es Salaam, anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Amina-Zahara Shabani Mtengeti (pichani) kilichotokea leo mei 31, 2014 katika hospitali ya Kinondoni - kwa Dkt. Mvungi.

Mazishi yamepangwa kufanyika kesho Jumapili baada ya swalat A'lasir katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Ataswaliwa msikiti wa Maamur, Upanga.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. Msiba upo nyumbani kwa Hajat Mwantumu Malale, Regent Estate.

INALILAHI WAINAILAIHI RAJIUN!!!


Post a Comment

1 Comments

  1. M.mungu ampe kauli thabit dada yetu mpendwa na kumuondolea adhab ya kabul wallah Allah ndio mjuwaji wa yote tuzidi kuombea dada Amina mpenzi wa watu

    ReplyDelete